Thursday, December 26, 2013

NASI TUMEKUJA KUMWABUDU.


PICHANI NI WANAKWAYA WA KANISA HILI LA VCC WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA MADHABAHUNI,picha na makitaba mwanzoni mwaka huu.
                                                NASI TUMEKUJA KUMWABUDU.
NA OSCAR SAMBA.
Hakika ni siku nyingine tena iliyosheheni utukufu mkuu wa MUNGU wetu wa mbinguni,Kwa jina la BWANA wetu YESU KRISTO nina kukaribisha katika makala hii inayo zungumzia Kuzaliw akwa YESU pamoja vitu muhimu vinavyo ambatana na sikuu hiyo.
Ujumbe huu umetolewa jana madhabahuni katika kanisa la VICTORY CENTRE LA TAG lililopo hapa mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR ES-SALAAM,      
Bila kupoteza muda na tutazame maandiko; MATHAYO 2:1-12.
Mpendwa ukisoma maandiko hayo utaona Yesu alivyozaliwa katika bethilehemu ya uyagudi enzi za mfaulme Herode,,Ukiendela utaona jinsi mamajusi walivyo tazama nyota na kwenda kumuona YESU pia walimtolea zawadi nyingi.
Wengine wanafikiria ni wanawake kwa sababu wanaitwa mamajusi na wengine wanazani ni mijusi,,MAMA JUSI NI WINGI UMOJA NI MAJAS,ndini ya ZOROTEANISM ilianzishwa Iran kabla ya YESU ilikuwa ni dini kubwa ya WAHAMEDI na WAHEDENI ambao makuhani wao waliitwa hivyo.
Walikuwa wakisomea elimu za nyota na zakishirikina za kusoma nyota.
Chakushangaza ni kwanini MUNGU alijifunua kwa watu hawa ,Ila nimegundu haya kwamba MUNGU humtumia mtu yeyote,

Tuesday, December 24, 2013

HATUA SABA ZA KUIMARUISHA USHIRIKA WAKO NA MUNGU.(maamuzi saba)

WAKWANZA KULIA NI MCHUNGAJI WA KANISA HILI LA VCC, ALOYCE MBUGHI NA WAPILI NI MAMA MCHUNGAJI CATHERINE MBUGHI NA MWINGINE NI MUUMINI WA KANISA HILI,picha na makitaba.
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha ewe mteule wa MUNGU wetu aliye mbinguni katika makala hii, ambayo inalenga kukujuza na kukuhabarisha njia kuu saba ambazo zitakusaidia kuimarisha mahusiano yako na MUNGU.
Ujumbe huu umetolewa leo madhabahuni katika kanisa la VICTORY CENTRE LA TAG lililopo hapa mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR ES-SALAAM,       KARIBU SASA.
Mstari wa kusimamia.
ZAB 27:4 Neno moja nimelitaka kwa Bwana  nalo ndilo nitakalolitafuta,nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za  maisha yangu niutazame uzuri wa BWANA nakutafakari hekaluni mwake.

1.Hatu ya kwanza [KWAME USIPOTEZE NJAA NA KIU YAKO KWA MUNGU,
Usimkinai MUNGU wala kumuona kama hana umuhimu,kwani adui akifanikiwa kuipoteza kiu na njaa hiyo atakupoteza kiimani.Pia kumbuka yya kwamba Mungu ndio dira yetu ukimpoteza utayumba na kuangamia,Usipoteze njaa na kiu mbele ya MUNGU wako ,usikate tama ewe mteule wa MUNGU.